Jeshi la Akiba Uvinza wasisitizwa mapambano dhidi ya uhalifu
KIGOMA: MKUU wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Mtela Mwampamba, amewaasa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wilayani humo kuwa mstari wa mbele katika mapambano mbalimbali ikiwemo dhidi ya vitendo vya kihalifu. Akizungumza wilayani humo Novemba 7, 2026 wakati akifunga mafunzo hayo kwa wahitimu 45 yaliyofanyika katika Kijiji cha Kandaga, Mwampamba amesema anaamini kupitia mafunzo hayo wahitimu hao watakuwa imara kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. “Niwapongeze kwa kuhitimu mafunzo haya lakini zaidi mnapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha vitendo vyote vya kihalifu ndani ya wilaya yetu na maeneo mengine havipati nafasi kwa maslahi mapana ya taifa letu,”amesema Mwampamba. Aidha, amevitaja baadhi ya vitendo hivyo vya kihalifu ambavyo kwa nyakati tofauti vimekuwa vikijitokeza ka…