08-11-2026

TanzaniaHabariLeo

TADB yaimarika, yadhamiria kuwafikia wakulima wadogo

DAR ES SALAAM: KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kuimarisha shughuli zake na kuongeza gawio kwa Serikali kutoka Sh500 milioni hadi Sh8.4 bilioni, hatua inayoonesha kuongezeka kwa tija katika usimamizi na matumizi ya mtaji wa umma. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ojambi Didas Masaburi, wakati wa kikao cha kamati kilichofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo wajumbe walipata fursa ya kutathmini majukumu, muundo wa kiutendaji na changamoto zinazoikabili benki hiyo. Masaburi amesema kamati hiyo ina wajibu wa kuhakikisha taasisi zinazopokea mitaji ya umma zinalinda uwekezaji huo, kuukuza na kuongeza tija kwa manufaa ya Watanzania. Ameeleza kuwa TADB imepiga hatua kubwa ikilinganishwa n…

Vichwa zaidi vya habari