08-11-2026

TanzaniaHabariLeo

Vijana 300 Muleba kupata fursa kilimo cha kahawa

MULEBA: Zaidi ya vijana na wanawake 300 wanatarajiwa kupata fursa za ajira na kipato kupitia kilimo cha kahawa katika Shamba la Vijana na Wanawake la Makongora, wilayani Muleba, mkoani Kagera. Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dk Abel Nyamahanga, amesema mradi huo ni sehemu ya jitihada za kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia sekta ya kilimo badala ya kutegemea ajira rasmi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), Dk. Nyamahanga amesema maandalizi ya shamba hilo yameanza kwa kusafisha mashamba na kuchonga barabara yenye urefu wa kilometa 20. Amesema kila kijana anaweza kupata mauzo ya kahawa yenye thamani ya hadi Sh milioni nane kwa msimu, iwapo atazingatia kanuni bora za kilimo. Kwa mujibu wake, shamba hilo lina uwezo wa kuvuna mara mbili kwa mwaka. A…

Vichwa zaidi vya habari