Serikali, wakandarasi kujadili kasi utekelezaji mradi wa SGR
TABORA: Serikali inatarajia kukutana ili kujadili mikakati ya kuharakisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokabiri mradi huo. Akizungumza alipokagua maendeleo ya ujenzi wa SGR kipande cha tatu katika eneo la Tura mkoani Tabora, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar alisema kikao hicho kitakachoongozwa na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba kitazikutanisha Wizara ya Fedha, Wizara ya Uchukuzi na wakandarasi lengo likiwa ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2028 ujenzi unakamilika. “Hivi karibuni tutakuwa na kikao cha pamoja kitakachoongozwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu ambacho kitazikutanisha wizara zote za kisekta pamoja na wakandarasi kujadili maendeleo ya ujenzi wa reli ya SGR,” alisema. Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alisema mkand…