TPC yaeleza umuhimu wa ofisi za usimamizi miradi
MOROGORO:Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeeleza umuhimu wa taasisi za umma kuwa na ofisi maalumu za usimamizi wa miradi, likisema mifumo hiyo inaweza kusaidia kuongeza ufanisi, uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kauli hiyo imetolewa katika Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Wataalamu wa Usimamizi wa Miradi Tanzania (PMI Tanzania Project Management Week & Annual Conference 2026), uliofanyika Novemba 5, 2026, katika Cate Hotel, Morogoro. Katika mjadala wa jopo kuhusu nafasi ya Ofisi za Usimamizi wa Miradi katika sekta ya umma, Meneja wa Ofisi ya Miradi wa Shirika la Posta Tanzania, Seleman Daffy, alishiriki kueleza uzoefu wa taasisi hiyo katika kutumia mfumo huo. Daffy amesema mjadala huo ulitoa fursa kwa taasisi mbalimbali kubadilishana uzo…