Bil 2/- kuwawezesha vijana, wanawake Kahama
KAHAMA: MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amekabidhi mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 2.167 kwa vikundi 96 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Kahama, akivitaka vikundi hivyo kuitumia fedha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukuza shughuli za kiuchumi na kujikwamua kimaisha. Fedha hizo zilizotokana na mapato ya ndani ya Manispaa ni sehemu ya asilimia 10 inayotengwa kwa ajili ya kuwawezesha makundi hayo kiuchumi. Akizungumza jana wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo hiyo, Mhita alisisitiza umuhimu wa vijana waliopata mikopo hiyo kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa kuzielekeza katika shughuli za uzalishaji badala ya kuzitumia katika anasa. Alisema mikopo hiyo inapaswa kuwa chachu ya kukuza biashara, kuongeza ajira na kuboresha maisha ya wanufaika, huk…